MVTTC Graduation Invitation!

Fomu ya Kudhibitisha Kuhudhuria Sherehe za Mahafali ya 26 Tarehe, 22-03-2024

Fomu ya Kudhibitisha Kuhudhuria Sherehe za Mahafali ya 26 Tarehe, 22-03-2024

TAARIFA YA SHEREHE YA MAHAFALI YA 26 NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA YA UALIMU WA UFUNDI STADI.

Mkuu wa Chuo kwa niaba ya Jumuiya nzima ya Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro (MVTTC) anayo furaha ya kuwaalika Wahitimu wa Mafunzo ya Ualimu wa Ufundi na Ufundi Stadi kwa Mwaka wa masomo 2021/2022 na 2022/2023 katika Sherehe ya Mahafali ya 26 ya Chuo iliyopangwa kufanyika tarehe 22 Machi, 2024 Kampasi Kuu, Chuo cha Ualimu wa Ufundi Stadi Morogoro kuanzia saa 4:00 asubuhi.

  • Astashahada ya Walimu Wasaidizi wa Ufundi Stadi Mkupuo wa Machi na Septemba 2021/2022.
  • Astashahada ya Walimu Wasaidizi wa Ufundi Stadi-Mafunzo Elimu Masafa Mkupuo wa Machi 2022/2023.
  • Cheti cha Msingi cha Ualimu wa Ufundi na Ufundi Stadi (NTA Level 5) Machi & Septemba 2021/2022.
  • Cheti cha Msingi cha Ualimu wa Ufundi na Ufundi Stadi (NTA Level 5) Mkupuo wa Septemba 2022//2023.
  • Stashahada ya Ualimu wa Ufundi na Ufundi Stadi (NTA Level 6) Mkupuo wa Machi & Septemba 2022/2023.

Je utashiriki Mahafali ya 26? *